Kocha Azam adai uchovu sababu kufungwa na Namungo

© Kwa Hisani

KANDANDA Kocha Azam adai uchovu sababu kufungwa na Namungo

Zahoro Mlanzi • 08:02 - 29.10.2023

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Azam wamefungwa mabao 3-1 na Namungo.

Kocha msaidizi wa timu ya Azam FC, Bruno Ferry, amesema uchovu kwa wachezaji wake ilikuwa ni sababu ya wao kufungwa mabao 3-1 nyumbani dhidi ya Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Ijumaa.

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Azam wamefungwa mabao 3-1 na Namungo.

Bruno amesema kwenye mechi dhidi ya Yanga ambayo pia walipoteza kwa mabao 3-2, walitumia nguvu kubwa na walikosa muda wa kujiandaa ili kucheza na Namungo.

Hata hivyo kocha huyo licha ya kuwa alikiri kwamba alama sita walizopoteza mfululizo ni muhimu lakini bado hawajatoka kwenye reli na lengo lao msimu huu.

"Uchovu ulitugharimu. Wachezaji walichoka baada ya mechi ya Yanga na pia wakakosa muda mzuri wa kujiandaa kuelekea mechi ya Namungo," amesema.

"Bado hatujatoka katika mstari wetu, tunaelekea kwenye mechi zijazo tukiwa na nguvu zaidi na malengo yetu msimu huu bado hayajabadilika," amemalizia.

Azam ambao sasa wanakalia kwenye nafasi ya tatu kwenye msimamo wakiwa na alama 13 wanatarajia kusafiri kwenda Kigoma kwa ajili ya kucheza na Mashujaa FC.