Azam FC yaitandika Green Warriors 4-0

Straika mpya wa Azam FC, Mcolombia Franklin Navarro (kulia), akimtoka mchezaji wa Green Warriors

KANDANDA Azam FC yaitandika Green Warriors 4-0

Zahoro Juma • 20:31 - 27.01.2024

Hiyo ilikuwa mechi ya kirafiki ambayo beki mpya wa Azam, Mcolombia, Yeison Fuentes, alipata nafasi ya kucheza

Timu ya Azam FC, leo imejaribu silaha zake mpya kwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Green Warriors na kuibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Mchezo huo uliofanyika Azam Complex jijini Dar es Salaam,wafungaji kwa upande wa Azam walikuwa ni Allasane Diao, Idd Nado, Nathan Chilambo na Zuber Foba.

Katika mchezo huo pia mchezaji mpya wa Azam, beki wa kati kutoka Colombia aliyesajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili, Yeison Fuentes alipata nafasi ya kucheza.

Azam walirejea kambini tangu wiki iliyopita na wamekuwa wakiendelea na mazoezi yao chini ya Kocha, Yusuph Dabo.

Hivi karibuni walitaka kasafiri kwenda kuweka kambi ya siku 10 visiwani Zanzibar lakini baadaye kambi hiyo ilifutwa.

Kwasasa timu hiyo ni vinara wa Ligi Kuu Bara, wakiwa na alama 31 na msimu huu wamepanga kurejesha furaha kwa mashabiki wao ambayo waliikosa kwa miaka 11.

Tags: