Bruno Ferry, amesema alitarajia kukutana na ushindani mkubwa kutoka kwa Dodoma lakini wanashukuru hawajafungwa.
Timu ya Azam FC, imekaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kutoka suluhu na Dodoma Jiji FC katika mchezo uliomalizika usiku huu Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Matokeo hayo yameifanya Azam kufikisha alama 10 ikifuatiwa na Yanga na Simba zenye alama 9 kila moja huku Dodoma ikifikisha alama 5 ikishika nafasi ya saba sawa na Tabora United.
)
08:15 - 03.10.2023
FOOTBALL AFCON 2027: The hundreds of millions Botswana splashed on bid book but lost to Kenya, Uganda and Tanzania
Botswana are counting losses running into hundreds of millions in the wake of their failed bid to secure the AFCON 2027 hosting rights
Mchezo huo ulitawaliwa na matumizi ya nguvu kutokana na kila upande kuikamia mechi ili kuondoka na alama tatu.
Azam itajutia nafasi iliyopata dakika ya 52 baada ya Lusajo Mwaikenda kufunga bao akiitendea haki pasi ya Idriss Mbombo lakini mwamuzi alidai ameotea na kuwafanya mashabiki wa Azam kujawa na hasira.
)
08:09 - 28.09.2023
FOOTBALL CAF insider reveals stadium selected for the 2027 Africa Cup of Nations final
CAF recently awarded Kenya, Uganda, and Tanzania the 2027 AFCON, with the three nations presenting a major stadium for the final.
Baada ya mchezo huo kumalizika, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Bruno Ferry, amesema alitarajia kukutana na ushindani mkubwa kutoka kwa Dodoma lakini wanashukuru hawajafungwa.
"Tulijua lazima mchezo utakuwa wa kasi na matumizi makubwa ya nguvu, wachezaji walipambana lakini haikuwa rahisi kwao kuondoka na alama tatu, tunajipanga kwa mchezo ujao," amesema Ferry.
)
21:00 - 03.10.2023
FOOTBALL 'Mane, Salah, Mahrez need more than just stadium!'- Jalango slams governors on AFCON venue
Lang'ata MP Jalang'o questions Western region's readiness for AFCON, highlighting the need for FIFA standards beyond stadium wishes.
Kwa upande wa Kocha Msaidizi wa Dodoma Jiji, Kassim Liogope, amesema alama moja waliyopata si haba mbele ya Azam FC kwani hiyo ni miongoni mwa timu kubwa nchini.
"Tuliisoma Azam katika mechi mbili za mwisho, tukajua ni wapi wana nguvu zaidi na kwenda kufanyia kazi kitu ambacho kimetusaidia kupata alama moja," amesema Liogope.
Ligi hiyo itaendelea Jumatano kwa mechi mbili ambapo Yanga itakuwa ugenini kuumana na Ihefu FC ikifuatiwa na mechi kati ya Kagera Sugar na Namungo FC.