Kocha Simba SC ahofia kuivaa KMC

LIGI KUU Kocha Simba SC ahofia kuivaa KMC

Zahoro Mlanzi • 15:35 - 22.12.2023

Timu hizo zitaumana kesho katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara

Kocha Msaidizi wa timu ya Simba SC, Seleman Matola, amesema wanatarajia mchezo mgumu dhidi ya KMC kutokana na ubora walionao msimu huu.

Timu hizo zinatarajia kuvaana kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam katika muendelezo wa michezo ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Matola amesema msimu huu KMC wameimarika zaidi na watachukuwa tahadhari zote wakati wanakabiliana nao uwanjani.

"KMC wamekuwa wakitupa upinzani mkali siku zote lakini msimu huu wameimarika zaidi hivyo tutaongeza tahadhari," amesema.

Aidha Matola amesema katika mchezo huo wachezaji wote wapo kambini isipokuwa Clotus Chama na Nassoro Kapama ambao wamesimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu.

Kwa upande wa Kocha wa KMC, Abdulhamid Moalin, amesema wanajua wanakutana na timu bora lakini watajitahidi kucheza kwa nidhamu kama walivyofanya mazoezi.

"Simba ni timu bora tunalijua hilo, tutajitahidi kucheza kwa nidhamu na kuondoa makosa ili tuweze kuvuna alama," amesema.

Tags: