Advertisement
KANDANDA

Rupia an'garisha Singida FG Ligi Kuu

© Kwa Hisani
Elvis Rupia ameifungia Singida Fountain Gate bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, wakisalia nafasi ya nane katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Advertisement

Straika Mkenya, Elvis Rupia, ameifungia bao pekee timu yake ya Singida Fountain Gate katika ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar, mchezo uliopigwa uwanjani Manungu mkoani Morogoro.

Advertisement

Mchezo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, umeifanya Singida FG kupanda hadi nafasi ya nane ikiwa na alama 5 huku Mtibwa ikiwa nafasi ya 14 kwa alama 2.

Rupia ambaye amesajiliwa na timu hiyo akitokea Polisi ya Kenya, hilo ni bao lake la pili tangu ajiunge na timu hiyo msimu huu.

Bao lake la kwanza alifunga katika michuano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Future ya Misri.

Advertisement

Straika huyo ambaye ni hodari katika upachikaji mabao,ndiye aliyekuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Kenya msimu uliopita akifunga mabao zaidi ya 25, amefunga bao hilo dakika ya 42 akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Nicolas Gyan.

Mchezo huo ambao ulihudhuriwa na mashabiki wachache, ulikuwa ni wa kuvutia kutokana na ushindani uliooneshwa na timu zote.

Advertisement