Advertisement

Taifa Stars wadhibitisha kuwa hawana hofu na kundi lao AFCON 2023

Wamewekwa kwenye kundi F katika michuano hiyo itakayofanyiwa mwakani nchini Ivory Coast kuanzia Januari 13 hadi Februari 11.
Advertisement

Saa chache baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kupanga ratiba ya michuano ya AFCON 2023, wachezaji wa timu ya Taifa (Taifa Stars), wamesema hawana hofu kupangwa kundi moja na Morocco, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Zambia.

Advertisement

Hilo ni Kundi F katika michuano hiyo itakayofanyiwa mwakani nchini Ivory Coast kuanzia Januari 13 hadi Februari 11.

Wakizungumza na Pulse sports kwa nyakati tofauti wachezaji wa Taifa Stars wakiwa wanajiandaa kwenda nchini Saudi Arabia kucheza mechi yao ya kirafiki dhidi ya Sudan, wamesema timu hizo walishacheza nazo kwa nyakati tofauti tofauti.

Winga, Simon Msuva ambaye anakipiga JS Kablie ya Algeria, amesema Zambia na DR Congo walishacheza nazo hivyo kikubwa ni kupambana kupata matokeo.

Advertisement

"Wachezaji tayari tuna uzoefu wa kutosha kwani tumeshacheza mechi nyingi ngumu, kikubwa ni kujituma na kulipambania Taifa letu lifanye vizuri," amesema Msuva.

Pia Mchezaji Kiraka, Novatus Dismas ambaye anakipiga Shakhtar Donetsk, amesema hawatokuwanll wanyonge katika Kundi hilo wapambana waone watavuna nini.

"Mpira siku hizi umebadilika hakuna tena kutishana katika majina makubwa, kikubwa ni kucheza kwa mpango na mbinu ili kupata matokeo," amesema Novatus.

Kwa upande wa Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Yanga na Ruvu Shooting, Charles Boniface Mkwassa, amesema hakuna kitu kinachoshindikana chini ya jua kikubwa ni maandalizi kwakuwa kundi hilo si jepesi.

Advertisement

Katika droo hiyo iliyopangwa jiijini Abidjan, Ivory Coast, Kundi A lina wenyeji Ivory Coast, Nigeria, Equatorial Guinea na Guinea-Buissau.

Kundi B linaundwa na Misri, Ghana, Cape Verde na Msumbiji, wakati Kundi C lina Senegal, Cameroon, Guinea na The Gambia.

Kundi G linazikutanisha Algeria, Burkina Faso, Mauritania na Angola wakati E kuna Tunisia, Mali, Afrika Kusini na Namibia.

Advertisement