Simba: Tutaishangaza Power Dynamos kwao

© Kwa Hisani

KANDANDA Simba: Tutaishangaza Power Dynamos kwao

Zahoro Mlanzi • 13:00 - 15.09.2023

Msafara wa mabasi hayo zaidi ya mawili yametoka jijini Dar es Salaam huku mabasi mengi yataungana nao mpakani Tunduma jijini Mbeya kwa ajili ya kwenda nchini humo.

Wakati baadhi ya mabasi ya mashabiki na wanachama wa Klabu ya Simba, leo wakianza safari ya kwenda Zambia, uongozi wa klabu hiyo, umetamba utaenda kuishangaza Power Dynamos kwa kuibuka na ushindi.

Msafara wa mabasi hayo zaidi ya mawili yametoka jijini Dar es Salaam huku mabasi mengi yataungana nao mpakani Tunduma jijini Mbeya kwa ajili ya kwenda nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa timu hiyo, Ahmed Ally ambaye yupo katika msafara wa mabasi hayo, amewashukuru wanachama na mashabiki hao kwa kujitokeza kwa wingi kwenda kuisapoti timu yao.

"Menejimenti na Bodi ya Simba inawashukuru kwa moyo huo wa kujitolea kwenda kuipambanai timu yao ugenini, na hatutawaangusha kwani tunakwenda kuitikisa Zambia kwa kuhakikisha tunaibuka na ushindi," amesema Ally.

Simba itaumana na Dynamos Jumamosi katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Levy Mwanawasa jijini Ndola ukiwa ni wa mkondo wa kwanza hatua ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Ni lazima Simba ipambane tuingine hatua ya makundi, malengo yetu si kupiga hesabu za makundi, huko tulishapita zamani sana, sasa hivi Simba ni timu kubwa lazima iwaze kikubwa, malengo yetu ni kufika mbali zaidi kuanzia robo hadi nusu fainali." ametamba Ally.

Kwa upande wa kiungo wa kimataifa wa Zambia, Clatous Chama, akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, amesema Dynamos ni timu nzuri na imekuwa ikibadilika kila mwaka, hivyo wanatakiwa kupambana kupata matokeo.

"Tulishacheza nao kama mara mbili na wamekuwa wakibadilika, tunatakiwa kujiandaa kwani mechi itakuwa ngumu sana, tuwaheshimu wapinzani wetu ili tuweze kufika mbali zaidi katika michuano hii," amesema Chama.